.
Azam FC ndiyo timu pekee ambayo imeruhusu magoli kuingia kwenye mechi moja tuu baada ya kukubali kutoka sare 2-2 na Toto Afrika jijini Mwanza huku ikiwa imeondoka bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye mechi tatu za ligi kuu.
Hadi kufikia raundi ya nne, Simba SC ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza pointi hata moja baada ya kucheza michezo minne na kushinda yote ambapo polisi Moro imejiwekea rekodi nyingine kwenye VPL raundi ya nne baada ya kuwa timu pekee iliyocheza mechi nne bila kufunga goli hata moja.
.
JKT Ruvu Stars ndiyo iliyoruhusu magoli mengi zaidi ya kufungwa ikiwa imefungwa magoli 10 hadi sasa ikifuatiwa na ndugu zao wa Ruvu Shooting Stars walioruhusu magoli nane kama ilivyo kwa wapiganaji wa African Lyon.
Kwa
upande wa magoli klabu ya Simba ndio inayoongoza ikiwa na magoli tisa
na kufuatiwa na Azam FC na Yanga pia yenye magoli saba huku vilabu vya
Ruvu Shooting Stars na Mtibwa Sugar vikiwa vimetikisa nyavu mara sita
kila kimoja.
Wachezaji Kipre Tchetche wa
Azam FC na Husein Javu wa Mtibwa na Nizar Khalfan ndiyo wanaoongoza
kufunga magoli kwenye ligi kuu wakiwa na magoli matatu kila mmoja hadi
hivi sasa.





0 comments:
Post a Comment